Serikali na upinzani waafikiana DR Congo

Askofu Marcel Utembi aliyeongoza majadiliano hayo amesema kuwa kuna changamoto chungu nzima mbele
Image caption Askofu Marcel Utembi aliyeongoza majadiliano hayo amesema kuwa kuna changamoto chungu nzima mbele

Maafisa wa serikali ya Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo, na makundi ya upinzani nchini humo wametia saini makubaliano yanayonuia kumaliza mzozo wa kisiasa unaogubika nchi hiyo.

Lakini ripoti zasema rais Kabila mwenyewe bado hajaweka saini yake.

Maaskofu kutoka kanisa katoliki waliokuwa wanaendesha shughuli hiyo ya upatanishi wanasema makubaliano ni kwamba rais Joseph Kabila anaweza kusalia madarakani kwa mda wa mwaka mmoja, lakini ni sharti uchaguzi ufanyike ndani ya kipindi cha miezi 12.

Sharti jingeni ni kuwa rais Kabila asiwanie tena kiti cha urais katika uchaguzi huo.

Image caption Rais Joseph Kabila wa DR Congo bado hajatia saini makubaliano hayo

Pia kiongozi mmoja wa upinzani anatarajiwa kuteuliwa kama waziri mkuu katika serikali ya mpito.

Mda wa utawala wa rais Kabila umemalizika mwezi huu lakini kutong'atuka kwake kumesababisha maandamano ambayo mara kwa mara yamekuwa yakikumbwa na ghasia ambapo watu zaidi ya 40 wamefariki.

Mada zinazohusiana