Watu 39 wauawa wakikaribisha mwaka mpya Uturuki

Mshambuliaji aliyetekeleza mashambulio hayo alitoroka na hajakamatwa hadi kufikia sasa Haki miliki ya picha AP
Image caption Mshambuliaji aliyetekeleza mashambulio hayo alitoroka na hajakamatwa hadi kufikia sasa

Takriban watu 39 wakiwemo wageni 15 wanahofiwa kuuawa katika shambulio la klabu ya burudani mjini Istanbul Uturuki, kulingana na waziri wa maswala ya ndani nchini humo.

Mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakijiburudisha katika mkahawa huo wa Reina saa saba usiku wakati ambapo watu walikuwa wakisherehekea kuingia kwa mwaka mpya.

Muuaji wa watu 39 katika kilabu ya burudani Uturuki asakwa

Urusi na Marekani zalaani shambulio Uturuki

Waziri huyo S├╝leyman Soylu ameelezea waliojeruhiwa kuwa 69 .

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kulingana na waziri wa maswala ya ndani takriban watu 39 wamefariki huku 69 wakijeruhiwa

Mtu huyo aliingia katika klabu hiyo akijifanya kikaragosi kilichovaa mavazi ya Santa Claus na punde kuanza kuwafyatulia risasi kiholela waliokuwepo.

Baadhi yao iliwabidi kujirusha baharini kuepuka msusuru wa risasi zilizokuwa zinafyatulia.

Polisi mmoja ni miongoni mwa waliofariki.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mtu huyo aliingia katika klabu hiyo akijifanya kikaragosi kilichovaa mavazi ya Santa Claus na punde kuanza kuwafyatulia risasi kiholela waliokuwepo.

Huku waliojeruhiwa wakikimbizwa hospitali, maafisa wa usalama wanaendelea kufanya upekuzi katika eneo hilo lakini muhusika wa shambilo hilo hajakamatwa bado.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii