Muuaji wa watu 39 katika kilabu ya burudani Uturuki asakwa

Polisi nchini Uturuki wamsaka mshambuliaji wa mkahawa wa Reina mjini Istanbul Uturuki
Image caption Polisi nchini Uturuki wamsaka mshambuliaji wa mkahawa wa Reina mjini Istanbul Uturuki

Maafisa wa polisi nchini Uturuki wanamsaka mshambuliaji aliyewafyatulia risasi watu waliokuwa wakisherehekea kuingia kwa mwaka mpya katika klabu moja ya burundani mjini Istanbul.

Waziri wa maswala ya ndani nchini Uturuki Suleyman Soylu anasema kuwa watu 39 wamefariki ikiwemo raia 15 wa kigeni huku zaidi ya watu 70 wakipelekwa hospitali na majareha .

Waziri huyo amekana madai kwamba kulikuwa na zaidi ya mtu mmoja aliyekuwa akiwafyatulia watu risasi kiholela.

Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan amesema kuwa mashambulio kama hayo yanalenga kuliyumbisha taifa na amewataka raia wa Uturuki kuungano dhidi ya kile lichokitaja kuwa ''mchezo mchafu''.

Mada zinazohusiana