Katibu mkuu mpya wa UN achukua mamlaka

Katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Image caption Katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres

Katibu mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ametoa wito kwa mwaka 2017 uwe wa amani.

Ikiwa ni siku yake ya kwanza katika wadhfa huo , Mr Guterres amesema lengo lake kubwa ni kusaidia mamillioni ya watu walioathiriwa na mogogoro wa kivita, akikumbusha kwamba maendeleo hayawezi kupatikana pasipo amani.

Hata hivyo katibu mkuu huyo anakabiliwa na changamoto nyingi , si tu kwamba kuna migogoro mingi duniani iliyosababisha kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi bali pia ukosefu wa nia njema ya kisiasa kutoka kwa rais mteule wa Marekani , Donald Trump ambaye juzi alitoa matamshi ya kuikashifu na kuipuuza kazi ya Umoja wa Mataifa.