Rubani apatikana mlevi kabla ya ndege kuondoka

Ndege hiyo ilitarajiwa kusafiri kutoka uwanja wa ndege wa Calgary Canada kuelekea nchini Mexico
Image caption Ndege hiyo ilitarajiwa kusafiri kutoka uwanja wa ndege wa Calgary Canada kuelekea nchini Mexico

Polisi huko Canada wamemkamata rubani mmoja aliyepatikana ,ndani ya ndege ya abiria kwenye chumba cha marubani akiwa amelewa chakari kwa mujibu wa vipimo alivyofanyiwa.

Rubani huyo alikuwa amepangiwa kuendesha ndege hiyo kwa safari ya kutoka uwanja wa ndege wa Calgary Canada hadi nchini Mexico ndipo lakini wafanyikazi wenzake wakamuona hakuwa katika hali sawa na kupiga ripoti.

Kisha punde baadae akaanguka na kuzirai.

Sasa amezindukia mashtaka ya kutaka kuendesha ndege akiwa mlevi na utovu wa nidhamu kazini.

Baadae rubani mwengine aliendesha ndege hiyo ya shirika liitwalo Sunwing iliyokuwa inaelekea Cancun mjini Mexico, ikiwa na abiria zaidi ya 100.

Mada zinazohusiana