Urusi na Marekani zalaani shambulio Uturuki

Rais Vladmir Puitin Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Vladmir Puitin

Nchi kadha zimelaani mashambulio hayo katika klabu ya starehe mjini Istanbul.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amesema ni shida kufikiria uhalifu mbaya zaidi, kushinda kuuwa raia wakati wanasherehekea mwaka mpya.

Ameahidi kuwa mshirika wa kuaminika wa Uturuki, katika mapambano yake dhidi ya ugaidi.

Nchini Marekani, Ikulu ililaani kile ilichokiita "ukatili wa shambulio la kigaidi".