Wafungwa 'magaidi' waachiliwa huru Bahrain

Taifa la Bahrain Haki miliki ya picha FRANK GARDNER
Image caption Taifa la Bahrain

Wakuu wa Bahrain wanasema wanaume waliokuwa na silaha wameshambulia gereza lenye wafungwa wahalifu na wale walioshtakiwa kufuatia na sheria za nchi kuhusu ugaidi.

Wiza ra mambo ya ndani ya nchi ya Bahrain, inasema kuwa askari polisi aliuwawa katika shambulio hilo dhidi ya Gereza Jaw, Kusini mwa mji mkuu, Manama.

Wizara inasema kwamba baadhi ya wafungwa waliokuwa kizuizini kwa sababu ya mashtaka ya ugaidi, wamekimbia.

Mwaka jana, wafungwa walifanya fujo katika gereza hilo huku wanaharakati wa haki za kibinaadamu wakidai kuwa baada ya ghasia kuzimwa, wafungwa waliadhibiwa.