Mlipuko wawaua watu 35 nchini Iraq

Takriban watu 35 wameuawa katika shambulio la kujitolea muhanga lililotokelezwa katika bustani maarufu iliopo katika mji mkuu wa Iraq Haki miliki ya picha AFP
Image caption Takriban watu 35 wameuawa katika shambulio la kujitolea muhanga lililotokelezwa katika bustani maarufu iliopo katika mji mkuu wa Iraq

Takriban watu 35 wameuawa katika shambulio la kujitolea muhanga lililotokelezwa katika bustani maarufu iliopo katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad kulingana na vyombo vya usalama.

Watu 61 wanadaiwa kujeruhiwa na mlipuko huo katika eneo la madhehebu ya Shia mashariki mwa mji wa Sadr.

Mlipuko huo ulitokea wakati ambapo rais wa Ufaransa Franswa Hollande alikuwa akivitembelea vikosi vya Ufaransa karibu na kambi moja mjini Baghdad.

Bw. Hollande amewaambia wanajeshi hao kwamba vita dhidi ya Islamic State nchini Iraq vinawasaidia kulinda mashambulizi ya kigaidi nyumbani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Hollande wa Ufaransa

Wapiganaji wa Islamic State wamesema kuwa walitekeleza shambulio hilo katika bustani maarufu mjini humo.

Bomu jingine lililotegwa ndani ya gari lililipuka katika gari karibu na hospitali ya Al-Kindi na kuwaua watu watatu.

Siku ya Jumamosi ,IS lilisema kuwa lilihusika na mashambulio mawili ya walipuaji wa kujitolea muhanga katika soko moja mjini Baghdad ambayo yalisababisha vifo vya watu 28.

Maeneo yaliolengwa ni yale ya Shia ambao inawataja kuwa waasi.