Israel:Benjamin Netanyahu ahojiwa kwa tuhuma za rushwa

Netanyahu amekana kuhusika katika tuhuma hizo
Image caption Netanyahu amekana kuhusika katika tuhuma hizo

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anahojiwa na polisi kwa tuhuma za ruswa zinazomkabili.

Netanyahu amekana kuhusika katika jambo hilo, huku akisema malalamiko yanayotolewa kwa yeye kupokea zawadi kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali ni uongo.

Televisheni imewekwa nyumbani kwake kuonyesha wapelelezi hao wakimuhoji.

Tekelezo hilo ni kwa amri ya mwanasheria mkuu wa Israel.

Image caption Netanyahu na Sara wamekuwa wakikosolewa mara kwa mara juu ya matumizi mabaya ya fedha za umma

Netanyahu na mke wake Sara wamehusishwa katika kashfa mbalimbali kipindi cha nyuma, ikiwemo tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za serikali.