kampuni ya magari ya Volvo yashindwa kuongoza kimauzo Sweden

Image caption Volvo imeongoza kimauzo kwa tarkibani nusu karne

Kwa mara ya kwanza ndani ya zaidi ya nusu karne, kampuni maarufu ya uuzaji magari nchini Sweden Volvo imeshindwa kuongoza kimauzo.

Kampuni hiyo ambayo kwa sasa inamilikiwa na kampuni ya kichina ya Zhejian Geely imeshindwa kutamba mbele ya kampuni nyingine ya Volkswagen Golf.

Mara ya mwisho Volvo kushindwa na kampuni la kigeni ilikuwa mwaka 1962, ambapo Volkswagen Beetle ilikuwa namba moja.