Trump apuuzilia mbali mpango wa Korea Kaskazini

Donald Trump asema kwamba Korea Kaskazini haitafanikiwa katika mpango wake wa kuunda kombora la masafa marefy litakalofika Marekani
Image caption Donald Trump asema kwamba Korea Kaskazini haitafanikiwa katika mpango wake wa kuunda kombora la masafa marefy litakalofika Marekani

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, amepuuzilia mbali madai ya Korea Kaskazini kuwa imeunda Kombora linaloweza kuwasilisha zana za nuklia hadi Marekani.

Katika mawasiliano kupitia mtandao wa Twitter, Bwana Trump aligusia majigambo ya kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, katika ujumbe wake wa mwaka mpya ambapo alisema kuwa maandalizi ya kombora la aina hiyo yamefikia hatua ya mwisho.

Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini

Korea Kaskazini yarusha makombora tena

Umoja wa Mataifa kuiwekea Korea Kaskazini vikwazo

Korea Kaskazini yaujaribu mtambo wa roketi

Bwana Trump alisema katika ujumbe wake kuwa "Haitawezekana." Tamko lake la haiwezekani, halikueleweka vizuri kwa sababu wachanganuzi hawajui iwapo alimaanisha kuwa Korea Kaskazini haina uwezo huo au alikuwa akiandaa hatua ya kujikinga.

Haki miliki ya picha Twitter
Image caption Ujumbe wa Twitter wa bwana Trump

Bwana Trump pia alishutumu Uchina kwa kushindwa kuthibiti mshirika wake Korea Kaskazini na pia akalaumu Beijing kwa kupokea pesa kiasi kikubwa cha pesa na mali kutoka Marekani.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii