Nkurunziza aonya kuwaondoa wanajeshi wake Somalia
Huwezi kusikiliza tena

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametangaza kuwa serikali yake inajiandaa Kuishtaki EU

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametangaza kuwa serikali yake inajiandaa kufungua mshataka baada ya hatua ya Muungano wa Ulaya kuzuwia mshahara wa vikosi vya Burundi vilivyoko nchini Somalia karibu mwaka mmoja sasa.

Kiongozi huyo wa Burundi ametishia kuyaondoa majeshi yake kwenye kikosi cha Amisom iwapo swala hilo halitapatiwa ufumbuzi.

Kutoka Bujumbura, muandishi wetu Ramadhani Kibuga anatuarifu zaidi.