Waasi wasitisha vita Msumbiji

Kinara mkuu wa vuguvugu la waasi nchini Msumbiji, Afonso Dhlakama Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kinara mkuu wa vuguvugu la waasi nchini Msumbiji, Afonso Dhlakama

Kinara mkuu wa vuguvugu la waasi nchini Msumbiji, Afonso Dhlakama, ametangaza usitishwaji wa mapigano kwa kipindi cha miezi miwili, huku akiongeza siku saba za mazungumzo ya amani, yalioanza msimu wote wa siku kuu ya krismasi.

Kinara huyo mkuu wa Vuguvugu la Renamo, na aliyechaguliwa kuwa kiongozi rasmi wa upinzani, aliongoza vita dhidi ya serikali ya Frelimo wakati wa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Msumbiji, ambayo yalimalizika mwaka 1992.

Hata hivyo mwaka jana, taharuki iliibuka tena na kumeshuhudiwa mapigano na mauwaji ya viongozi wa kisiasa.

Bwana Dhlakama sasa anaishi mafichoni katika maeneo ya milima katikati mwa nchi hiyo.