Shambulizi la anga laua watu 25 Idip Syria

Baadhi ya sehemu zilizoathiriwa na shambulizi hilo
Image caption Baadhi ya sehemu zilizoathiriwa na shambulizi hilo

Wanaharakati nchini Syria wanasema shambulizi la anga limegonga jengo lililokuwa likitumiwa na waasi wa kundi la jihadi kaskazini mwa jimbo la Idlip na kuuwa watu ishirini na tano.

Waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria wamesema ndege iliyotumika haijatambulika.

Shambulio hilo lililenga Jabhat Fateh al-Sham iliyokuwa inajulikana kama Nusra Front ambapo zina ushirikiano na al-Qaeda.

Urusi na Syria zimesema kundi hilo halihusiki na mpango wa kusitisha mapigano ulioandaliwa nchini syria.