Trump asababisha Ford kuacha kutengenezea magari Mexico

Trump aliikosoa kampuni hiyo mapema jumanne kwa kutengeneza magari Mexico na kuyaingiza bure Marekani
Image caption Trump aliikosoa kampuni hiyo mapema jumanne kwa kutengeneza magari Mexico na kuyaingiza bure Marekani

Kampuni kubwa ya magari nchini Marekani Ford, imetangaza kwamba itaachana na mpango wake wa kutaka kutengeneza kampuni ya magari nchini mexico itakayogharimu dola Bilioni 1.6 ili kuwekeza zaidi nchini Marekani.

Mark Fields ambaye ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Ford amesema maamuzi hayo ni matokeo ya kura ya Imani ya wanaounga mkono biashara iliyokuwa ikiundwa na Donald trump.

Wakati wa kampeni za kuwania kiti cha Urais bwana Trump aliikosoa vikali kampuni ya Ford kwa kupeleka shughuli za utengezaji wa magari nchini Mexico na kutishia kuanzisha ushuru kwa magari yatakayotengenezwa nje ya mipaka na kuuzwa nchini Marekani.

Mapema siku ya jumanne ametoa tishio sawa na hilo kwa kampuni ya General Motors.