Wabunge Republican kutoikamata tume ya maadili Marekani

Mpango huo ulikuwa unaungwa mkono na mjumbe mkuu wa Congress Bob Goodlatte kushoto
Image caption Mpango huo ulikuwa unaungwa mkono na mjumbe mkuu wa Congress Bob Goodlatte kushoto

Wabunge wa upinzani katika bunge la Marekani,wameondoa makubaliano yaliyokuwa na utata ya kuikamata tume huru ya maadili inayofuatilia mamlaka yake.

Mpango huo umewakasirisha wanachama wa Democratic na umekosolewa na Rais mteule wa Marekani Donald Trump ambapo alisema ilikuwa sio kipaumbele.

Katika mtandao wa tweeter Donald Trump alipendekeza kwamba,mabadiliko katika suala la kodi na huduma za afya ndicho kipambele kikubwa kwa chama cha Republican.

Mwandishi wetu anasema ni aibu kwa chama na inaonyesha ukosefu wa umoja.

Wakati huohuo Mike Enzi ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya bajeti wa Republican katika bunge la Marekani , ameanzisha azimio la kutaka kufuta sheria ya Afya ya Barack Obama.

Mchakato wa kufuta sheria hiyo unaweza kuchukua miezi na mchakato wa kuanzisha mpango mpya wa bima ya afya unaweza kuchukua hata miaka.