Tathmini ya mwaka wa mwisho wa rais Obama madarakani kwa picha

Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mnamo mwezi Februari: "Mpiga picha huyu anampata rais Obama akiwaza ,kitu ambacho si rahisi kuangazia .Alikuwa akijiandaa na wafanyikazi wake wa usalama kabla ya mkutano na viongozi wa Ulaya.
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Februari: "Rais Obama ashtuka baada ya mpira wake wa gofu kushindwa kuingia katika shimo la mchezo huo
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Machi: "Ni heshima isio kifani kuwaona wasichana hawa wakikuwa. Malia aliye mbele na Sasha wote walialikwa kuwa wageni wa chakula cha jioni kwa heshima ya waziri mkuu wa Canada Trudeau Justin.
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Machi: "Ni mchana mmoja ambapo rais Obama alianza kucheza densi mbele ya msaidizi wake wa ikulu Ferial Govashiri alimuonyesha kusakata densi akijiandaa kwa harusi yake''
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Machi: Mke wa rais Obama anaangalia huku rais Obama akimpa pambaja Caprina Harris. Caprina alidaiwa kulia aliposikia kwamba rais Obama hatokuwa tena rais, video hiyo iliokuwa katika mtandao wa Yu Tube ilisambazwa sana na rais Obama akamjibu kupitia mtandao wake wa facebook na kusema hendi kokote. Ni sababu hiyo iliosababisha wao kukutana.
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwanamfalme George asalimia kwa mkono na rais Barrack Obama aliyechuchumaa ,huku mkewe rais Obama na babake George mwanamfalme William akiangalia.
Haki miliki ya picha David Lienemann / White House
Image caption Mwezi June: Makamu wa rais wa Marekani Joe Bidden awafukuza watoto na waandishi habari kwa kutumia maji kwa jina super soaker wakati wa sherehe yake iliofanyika Washington DC
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Juni: Mtoto wa kike aliyekalia kiti cha makamu wa rais amwangalia rais Obama ambaye pia naye akimatzama na kutabasamu
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Julai: Angela Merkel, katikati, akicheka huku mikono yake ikiwa mdomoni ,naye rais wa Ufaransa Francois Hollande kushoto na Obama wakikosa kuonyesha hisia.
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Agosti: Huku wafanyikazi wakiangalia ,rais Obama alizima mishumaa iliowekwa katika zawadi ya keki ya siku yake ya kuzaliwa
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Agosti: Nje ya ofisi ya Oval nchini Marekani, rais Barrack Obama anaangalia filamu kupitia miwani ya Virtual Reality huku msaidizi wake akimpuuza na kuendelea na kazi yake.
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Septemba: Rais Obama alikuwa ameenda kutembea na mwanawe Malia katika mbuga ya wanyama ya Great Falls mjini Virginia na kukalia mwamba karibu na mto Potomac.
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Septemba: Baada ya kukutana na muigizaji na mwanaharakati wa haki za kibinaadamu George Clooney, rais alimualika yeye na wenzake watatu ili kupiga filamu ya Hoops katika eneo la kuchezea mpira wa vikapu la ikulu ya White.
Haki miliki ya picha Lawrence Jackson / White House
Image caption Mwezi Septemba: Mke wa rais Michelle Obama akiwa katika duka la jumla tayari kujiandaa kwa maisha baada ya ikulu ya Whitehouse mjini California.
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Septemba: Rais Obama ampiga picha aliyekuwa rais George Bush na mkewe laura Busha katika hafla ya ufunguzi wa makavazi ya Waafrika Wamarekani .
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Oktoba: Rais Obama anaketi katika benchi katika Ikulu ya Whitehouse akizungumza na mtu bandia .
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Oktoba: Kulikuwa hakuna mwangaza wakati rais Obama na mkewe walipokuwa wakitembea ndani ya Ikulu ya Whitehouse kwa mkutano wa mwisho wa mwaka na wafanyikazi wa Ikulu hiyo.
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Oktoba : Rais Obama alikuwa anawakaribisha watoto walio jirani na Whitehouse kwa sherehe ya halloween wakati alipokutana na mvulana huyu aliyekuwa amevalia kama Superman. furisha misuli yako,Obama alimwambia mvulana huyo.
Haki miliki ya picha Pete Souza / White House
Image caption Mwezi Novemba: Rais Obama akutana na mvulana aliyemwandikia barua akimtaka kumnusuru kijana wa Syria aliyepatikana chini ya vifusi vya jumba lililolipuliwa mjini Allepo Syria. Kijana huyo alimtaka rais Obama kumchukua mvulana huyo na kumpeka kwao.