Rais wa Kenya akutana na wahudumu wa matibabu waliogoma

Wahudumu wa matibabu waliogoma kutokana na kukosa nyongeza ya mishahara
Image caption Wahudumu wa matibabu waliogoma kutokana na kukosa nyongeza ya mishahara

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amekutana leo na wataalamu wa kimatibabu, ambao wamekuwa wakigoma kwa zaidi ya mwezi mmoja, ili kutafuta suluhu ya maandamano hayo ambayo yamelemaza shughuli za matibabu nchini humo.

Madaktari na wafanyikazi wengine wa afya, wanasema kuwa mamlaka kuu nchini humo, bado haijatimiza makubaliano yao ya nyongeza ya mishahara na mafao mengine walioafikiana mwaka 2013 walioahidiwa.

Mgomo huo umeathiri pakubwa sekta ya afya nchini Kenya, huku baadhi ya wagonjwa wakifariki kwa sababu ya kutohudumiwa kimatibabu.