Waziri atimuliwa kwa kutaka kumkaribisha Trump Mexico

Rais Enrique Pena Nieto
Image caption Rais Enrique Pena Nieto

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, amemteuwa aliyekuwa waziri wa fedha Bwana Luis Videgaray, kuwa waziri mpya wa mambo ya kigeni.

Bwana Videgaray ni moja kati ya watu wake wa karibu ingawa alitimuliwa mwezi Septemba wiki moja baada yakupanga na kumkaribisha Donald Trump kutembelea Mexico.

Alikosolewa kwa kumkaribisha mgombea wa kiti cha Urais wa Marekani aliyekuwa akikosoa wahamiaji kutoka Mexico.

Rais huyo wa Mexico amesema Videgaray alishtakiwa kwa kuboresha mazungumzo na uongozi ujao wa Marekani.