Utamaduni wa kutoa majina Afrika: Njia tisa za kumpatia jina mtoto wako

Utamaduni wa kutoa majina Afrika: Njia tisa za kumpatia jina mtoto wako Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Utamaduni wa kutoa majina Afrika: Njia tisa za kumpatia jina mtoto wako

Majina yanayotokana na utamaduni wa Kiafrika hushirikisha hadithi fulani.

Kutoka siku mtoto anapozaliwa hadi matukio yanayozunguka kuzaliwa kwake, sababu kadhaa hushawishi majina ambayo wazazi huwachagulia watoto wao.

Kila kabila, majina hayo huwa na habari nyingi kumuhusu mtu aliyepewa jina hilo.

Hizi ni njia tisa tofauti ambazo wazazi wa Kiafrika hutaja majina ya watoto wao:

1. Matukio yanayozunguka kuzaliwa:

Miongoni mwa makabila tofauti uchaguaji wa majina unaweza kushawishiwa na matukio mazuri ama hata mabaya ambayo familia hujikuta ndani yake wakati mtoto anapozaliwa.

Mara nyingi majina hayo huwa na sentensi:

Ayodele{ furaha imekuja nyumbani} ni jina linalotumiwa na jinsia zote mbili kwa mtoto ambaye kuzaliwa kwake kumeleta furaha kwa wazazi wake wa kabila la Yoruba nchini Nigeria.

Yetunde ama Yewande {Mama amerudi} ni Jina la kabila la Yoruba linalopatiwa mtoto wa kike ambaye bibiye au mwanamke mwengine wa familia yake alifariki kabla ya kuzaliwa kwake.

Adetokunbo (Ufalme ama utajiri umerudi nyumbani) ni jina linalotumika na jinsia zote kwa mtoto aliyezaliwa ughaibuni.

Haki miliki ya picha Yetunde Nwaokeke
Image caption Yetunde {amerudi} ni jina analopatiwa mtoto linalofana ana bibi miongoni mwa raia wa Nigeria

Ajuji {aliyezaliwa katika jaa} ni jina linalopatiwa mtoto baada ya watoto waliozaliwa mbele yake kushindwa kuishi.

Inaaminika kwamba kumpatia mtoto jina baya kutawadanganya mapepo wabaya kudhani kwamba mtoto huyo hapendwi hatua itakayowafanya mapepo hao kumwacha kuishi.

Kgomotso na pumza{faraja} ni majina yanayopewa watoto wanaozaliwa muda mfupi baada ya kifo ama hata janga katika familia za Sesotho na Xhoza nchini Afrika Kusini.

Kiptanui na Cheptanui ni majina yanayopewa watoto ambao mama yao amekumbwa na matatizo mengi wakati wa kujifungua miongoni mwa jamii ya Wakalenjin nchini Kenya.

Kimaiyo na Jemaiyo ni majina ambayo mara nyengine hupewa watoto wa kiume na wa kike ambao kuzaliwa kwao kunajiri wakati ambapo wanaume wanakunywa pombe ya Maiywek miongoni mwa Wakalenjin.

Misrak {mashariki} ni jina lililopewa mtoto wa kike wa Ki-Ethiopia ambaye babake alitoka Japan wakati alipozaliwa.

Lindiwe {Tumesubiri} ni jina la Kizulu linalopewa mtoto wa kike baada ya kuzaliwa kwa wavulana wengi.

2. Onyo lenye hisia:

Baadhi ya majina ,hususan kutoka nchini Zimbabwe ,yanaonyesha hali matukio yanayokumba familia wakati wa kuzaliwa.

Mengine hutoa tahadhari ama hata kukemea.

Nhamo Inamaanisha bahati mbaya.

Maidei anauliza swali ulitaka nini?

Yananiso ina maanisha kuleta familia pamoja.

3. Mara nyengine majina haya hutafsiriwa Kizungu ambapo hutoa maana ya kushangaza,kwa mfano:

Airfoce: Kissmore: Brilliant: Psychology: Hatred: Nomatter; Jealous; Furious au Hardlife.

Lakini sio jambo la kipekee kwa raia wa Zimbabwe.

Gospel Mavutula kutoka taifa jirani la Malawi alikuwa ameitwa jina Misery lakini akaamua kwamba jina hilo lina maana mbaya na kulibadilisha.

''Nilizaliwa katika kipindi ambacho wazazi wangu walikuwa na matatizo," aliambia BBC.

Anasema kuwa wazazi wake ambao wote ni walimu walipata shinikizo kali kutoka kazini na matatizo na majirani zao na hilo ndilo lilishawishi kuzaliwa kwangu.

Image caption Gospel Mavutula anasema kuwa maisha yake yalibadilika baada ya kubadili jina Misery alilopewa

''Nimeamua kupuuzilia mbali hali hiyo kwa kuwapatia majina mazuri watoto wangu'', aliongezea.

Na katika jimbo la Volta nchini Ghana, wapenzi wawili wanaotoka katika kabila la Ewe waliamua kuwacha kupata watoto lakini wakajifungua mtoto wao wa mwisho wa kike.

Ili kuonyesha kuwa mtoto huyo alikuja kwa bahati mbaya waliamua kumuita Melevevio ikimaanisha kwamba sio muhimu.

4. Utamaduni wa watu maarufu:

Kabila la Wajaluo nchini Kenya linajulikana kwa kuwapatia majina maarufu watoto wao.

Baadhi ya akina mama waliwataja wana wao wavulana Obama 2008 baada ya rais huyo wa Marekani, mwana wa mwanamume mjaluo kuchaguliwa kuwa rais.

Na alipotembelea taifa hilo mwaka 2015 mwanamke mmoja alimtaja mwanawe jina Airforceone.

Majina ya Churchill na Clinton ni majina maarufu sana katika maeneo ya kabila la Waluo.

Kuna mzazi aliyemtaja mwanawe jina la Donald Trump Otieno .

Wazazi wake waliambia Nairobi News waliamua kumuita mwana wao baada ya rais huyo mteule wa Marekani kwa sababu walipendelea sana sera za mfanyibiashara huyo bilionea.

Lakini kutajwa kwa watoto kulingana na majina ya watu maarufu katika habari sio jambo geni miongoni mwa Waluo nchini Kenya.

5. Utaratibu wa kuzaliwa:

Katika tamaduni nyingi, hakuna haja ya mtu kuelezea kwamba yeye ndio aliozaliwa kwanza au mwisho.

Hii ni kwa sababu majina yao yanaweza kubaini hilo. Hii hususan huonekana miongoni mwa mapacha.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watoto mapacha wafanyiwa tambiko fulani

Iwapo utakutana na mvulana kutoka Uganda ama mtu kwa jina kakuru ama Waswa, kuna uwezekano anaweza kuwa pacha mkubwa.

Pacha mdogo wa kiume anaitwa Kato. Haya ni majina yanayohifadhiwa mapacha.

Vilevile, kabila la Wakalenjin nchini Kenya humuita mtoto wa kwanza Yator (kifungua njia) na mwana wa mwisho Towett ikimaanisha mwisho.

Watu wa kabila la Yoruba humuita pacha wa kwanza Taiwo (Onja ulimwengu) na wa pili Kehinde (alikuja baada ya}).

Nchini Ghana, majina yanayotumiwa na jinsia zote Panyin na Kakra ambayo humaanisha mkubwa na mdogo hutumiwa kwa mapacha.

6. Majina ya kuzaliwa mchana:

Hata kabla ya wazazi kuchagua jina la magharibi ama la kidini kwa watoto wao, mwana huyo tayari huwa na jina.

Miongoni mwa makabila ya Ghana kama vile Akan, Ga, Ewe na Nzema, jina hutumiwa kulingana na siku ya mtoto aliozaliwa. Siku hizi majina hulingana na siku ya wiki mtoto aaliyozaliwa na kwa hivyo kila mtu ana jina moja ijapokuwa jina hilo ni nadra kuliona katika vyeti rasmi.

Haki miliki ya picha AMFO Connolly
Image caption Mzaliwa wa Canada fue aliyezaliwa siku ya Ijumaa hakupewa jina la Magharibi

Jumatatu- Kojo (mume), Adwoa (mwanamke)

Jumanne - Kwabena (mume), Abena (mwanamke)

Jumatano - Kwaku (mume), Ekua (mwanamke)

Alhamisi- Yaw (mume), Yaa (mwanamke)

Ijumaa - Kofi (mume), Efua (mwanamke)

Jumamosi - Kwame (mume), Ama (mwanamke)

Jumapili- Akwesi (mume), Akosua, (mwanamke)

Miongoni mwa makabila mashariki na kusini mwa Afrika, majina fulani huchaguliwa kulingana na muda ama siku ama hata msimu mtoto anaozaliwa.

Kibet humaanisha siku na Kiplagat humaanisha usiku miongoni mwa Wakalenjin nchini Kenya.

Mumbua na Wambua humaanisha msimu wa mvua miongoni mwa wavulana na wasichana katika kabila la Wakamba nchini Kenya.

Olweny humaanisha wakati wa vita miongoni mwa watu wa kabila la Luo.

Yunwa humaanisha njaa ama wakati wa njaa miongoni mwa watu wa kabila la hausa nchini Nigeria.

7. Miongoni mwa Wajaluo:

Omondi (alfajiri)

Okinyi (asubuhi)

Onyango (mchana)

Ochieng' (mchana ulio na juwa jingi)

Otieno (usiku)

Oduor (saa sita ya usiku)

Wasichana hupewa majina kama hayo lakini yanayoanza na herufi A badala ya O.

8. Wasomali nao huwa na mfumo wa kipekee:

Wengi wao huwa na majina matatu - waliopatiwa pamoja na yale ya baba yao na babu.

Image caption Justin Marrozi {Timo Cade}

Lakini wengi pia huwa na majina ya kutungwa, ambayo hujulikana hali ya kwamba yanaweza kutumika katika vitambulisho vyao.

Majina haya hulingana na maumbile ya mtu alivyo.

Baadhi ya majina hayo ni Langare (anayeguchia), Coryaan (mlemavu), Lugay (mtu mwenye mguu mmoja), ama Genay (anayekosa jina moja) hatahivyo wanawake hupata majina mazuri kama vile Lul (almasi), Macnay (peremende), Cod Wayne (aliye na sauti nzuri), Dahable (Dhahabu) na Indho Daraleey (mwenye macho ya paa).

9. Miongoni mwa Waswahili mkoa wa Pwani Tanzania

Majina haya mara nyingi utolewa na baba wa watoto ili kujibu maswali ambayo wanakuwa wanajiuliza wakati wa ujauzito au mahusiano yao

Mashaka: Mzazi wa kiume anakuwa na kitu fulani kama pingamizi au wasiwasi ambao hutokana na mzozo kati yake yeye na mkewe hivyo mtoto anapozaliwa hupewa jina hilo la Mashaka yaani wasiwasi. (Mtoto wa Kiume)

Fikiri: hili linatolewa na mume huku likimtaka mke atafakari tabia zake (Mtoto wa kiume na kike).

Mkegani: Jina hili anapewa kwa mtoto ambaye amezaliwa kwa mke ambaye mume hakutarajia kumuoa, na labda alifungishwa ndoa ya mkeka au ujauzito ulimlazimu amuoe huyo binti, hivyo badala ya kumwambia mke wake kuwa yeye hakuwa chaguo lake anaamua kumpa mtoto wa kike atakayezaliwa jina hilo

Si wazuri: Jina hili ni la msichana ambalo linatolewa kama ujumbe kwa majirani ambao hawakutegemea kuona wazazi hao watazaa

Shida: Hali ya kiafya ya mama mtoto wakati yuko mjamzito ilikuwa sio nzuri, au alipata ujauzito kwa kuhangaika sana na hata wakati wa kujifungua mama alikutana na wakati mgumu sana lakini vilevile ugumu wa hali ya maisha unaweza kupelekea jina hilo kutolewa

Mkambara: Ni mti mmoja mrefu sana

Maneno: Familia za pande zote mbili walikuwa wanazungumza sana kuhusu mahusiano yao au ndoa yao hivyo ujumbe wa kuwafahamisha kuwa maneno yao wameyasikia baba analitoa jina hilo kwa mtoto.