Marekani: Ilikuwa ajabu Urusi kuingilia uchaguzi wa 2016

Urusi inalalamikiwa kudukua taarifa za uchaguzi wa Marekani 2016
Image caption Urusi inalalamikiwa kudukua taarifa za uchaguzi wa Marekani 2016

Mkurugenzi wa usalama wa Marekani James Clapper, kitendo cha Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita kilikuwa cha ajabu kushuhudia katika utendaji kazi wake.

Akizungumza katika Baraza la senate Nchini Marekani, Clapper amesema udukuzi huo wa barua pepe za chama cha Democratic kuelekea uchaguzi uliofanyika mwezi Novemba ulisimamiwa na Raisi wa Urusi Vladimir Putin, na kuongeza kuwa atatoa taarifa kamili kwa umma wiki ijayo.

Image caption Mkurugenzi wa usalama wa Marekani James Clapper

Clapper amesema kuwa ifikapo ijumaa atatoa mchanganuo wa tafiti zake kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump aliyewahi kulaani na kutilia shaka ushiriki wa Moscow.

Urusi pia imekanusha madai ya kuhusika katika udukuzi huo.