Wahalifu wawakata vichwa wafungwa 33 Brazil

Familia za wafungwa zinasema hadi wafungwa 40 huenda waliuawa Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Familia za wafungwa zinasema hadi wafungwa 40 huenda waliuawa

Genge moja la uhalifu linaloendesha shughuli zake katika magereza mbalimbali nchini Brazil, limewakata vichwa takriban wafungwa 33 katika gereza moja katika jimbo la Kaskazini la Roraima.

Ni tukio la pili chini ya juma moja kutokea nchini Brazil.

Maafisa wa Serikali wanaamini kuwa kukatwa vichwa huko kunatokana na mzozano unaondelea miongoni mwa wanachama wa genge hilo lijulikanalo kama PCC.

Gereza hilo lililosongamana liko eneo la mashambani, nje ya mji mkuu wa jimbo wa Boa Vista.

Hadi kufikia sasa maiti 31 zimepatikana. nyingi ya maiti hizo zimekatwa vichwa au kukatwakatwa vipande.

Maafisa wa Serikali wanasema ghasia hizo ni sehemu ya juhudi za magenge kuwa na mamlaka katika baadhi ya magereza.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kwa sasa polisi wamechukua udhibiti wa gerea hilo
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanachama wa magenge tofauti huzuiwa katika sehemu tofauti za gereza