Jeshi la Iraq lakaribia kudhibiti mji wa Mosul

Wanajeshi wa Iraq wamepata ushindi tangu oparesheni ianze mwezi Oktoba mwaka uliopita Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa Iraq wamepata ushindi tangu oparesheni ianze mwezi Oktoba mwaka uliopita

Wanajeshi wa Iraq wanaojaribu kuwatoa wapiganaji wa Islamic State mjini Mosul, wanasema sasa wako kama mita mia chache tu kutoka mto Tigris, ambao unagawa mji huo.

Siku za karibuni, jeshi la serikali limesonga mbele upande wa mashariki ya Mosul, baada ya ku-kwama kwa majuma kadha.

Leo asubuhi, jeshi lilisema limeuteka mtaa wa Al-Ghofran.

Islamic State bado inadhibiti sehemu kubwa ya mji wa Mosul, ulioko ufukwe wa magharibi ya Mto Tigris.

Oparesheni ya kuuteka mji wa Mosul ilianzishwa tarehe 17 mwezi Okotoba, baada ya zaidi ya miaka miwili tangu wapiganaji kuudhibii mji huo.

Wanajeshi wa Iraq, wapiganaji wa kurdi na wale wa shia, wakisaidiwa na muuangano unaoongozwa na Marekani wamekuwa wakishiriki mapigano hayo.

Zaidi ya watu 100 wamekimbia makwao ndani na nje ya Mosul.