Wanajeshi waliogoma wamuachilia waziri Ivory Coast

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi waliogoma wakisimama nyuma ya waziri wa ulinzi Alain-Richard Donwahi (aliyeketi kati kati)

Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, amesema kuwa maafikiano yametimizwa ili kumaliza uhasama ndani ya jeshi la taifa hilo.

Bwana Ouattara, amesema kuwa wanajeshi waliokuwa wakishinikiza kulipwa marupurupu yao, watalipwa huku akiwaomba kurejea katika kambi zao.

Waziri wa ulinzi wa Ivory Coast, Alain-Richard Donwahi ambaye alikuwa amezuiliwa na wanajeshi hao ameachiwa huru.

Wanajeshi waandamana Ivory Coast

Uchaguzi Ivory Coast: Upigaji kura wachelewa

Bwana Donwahi amekuwa akiendesha majadiliano katika mji wa Bouake, ulioko katikati mwa nchi hiyo, tangu siku ya Ijumaa.

Haijafahamika ikiwa wanajeshi hao wote, watakubali kuelewana na serikali.