Aliyewaua watu 5 Marekani afunguliwa mashtaka

Mshukiwa Esteban Santiago ni mwanajeshi wa zamani
Image caption Mshukiwa Esteban Santiago ni mwanajeshi wa zamani

Mwanajeshi wa zamani nchini Marekani anayeshukiwa kuwauwa watu watano katika uwanja wa ndege wa Fort Lauder-dale huko Florida siku ya Ijumaa, amefunguliwa mashtaka ya kuuwa na kusababisha majeraha kwa kutumia silaha.

Sasa huenda Esteban Santiago, akakabiliwa na hukumu ya kifo.

Mamlaka kuu nchini Marekani, inakabiliwa na maswali magumu, baada ya FBI kukiri kuwa Bwana Santiago, alizuru ofisi zake huko Alaska mwezi Novemba, na akawasilishwa katika hospitali ya matatizo ya akili, ili apimwe.

Kakake Santiago, Brayan, anataka kujua kwa nini mamlaka kuu ilisema hivyo, lakini haikuchukua hatua zozote.

Polisi wa Alaska, sasa wanasema kwamba, hawange mpokonya bunduki Bwana Santiago, wakati huo, kwa sababu hakuwa ametekeleza uhalifu wowote.

Haijabainika ikiwa bunduki hiyo ndio iliyotumika katika uhalifu kwenye uwanja huo wa ndege.The man suspected of carrying out a deadly shooting at a Florida airport has been charged by prosecutors.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Watu wakijikinga nyuma ya magari

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii