Mlipuko wawaua 11 Baghdad

Mlipuko huo ulitokea kwenye soko moja mjini Baghdad Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mlipuko huo ulitokea kwenye soko moja mjini Baghdad

Taarifa kutoka mji mkuu wa Iraq, Baghdad, zinasema kuwa mshukiwa mmoja mlipuaji wa kujitolea mhanga, amejilipua ndani ya gari katika lango la kuingia kwenye soko moja kuu la kuuzia mboga mjini humo.

Watu 11 wameuwawa na zaidi ya hamsini wamejeruhiwa katika mlipuko huo.

Soko hilo liko katika eneo lililo na waislamu wengi wa-kishia, katika Wilaya ya Jamila.

Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na mlipuko huo, lakini katika kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita, Kundi la Islamic State, lilikiri kupanga na kutekeleza mashambulio kadhaa katika mji huo mkuu.

Hilo ndilo shambulizi la hivi punde linalolenga mitaa ya washia wengi. Shambulizi sawa na hilo lilitokea tarehe mbili mwezi huu na kuwaua watu 35.

Image caption Baghdad