Buhari kuongoza mazungumzo kuhusu Gambia

Bwana Buhari na viongozi wengine wa nchi za Afrika Magharibi walimtembelea bwana Jammeh mwezi uliopita Haki miliki ya picha EPA
Image caption Bwana Buhari na viongozi wengine wa nchi za Afrika Magharibi walimtembelea bwana Jammeh mwezi uliopita

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anandaa mkutanao wa viongozi wanne wa nchi za Afrika Magharibi baadaye leo katika jitihada za kuzuia kutokea ghasia nchini Gambia.

Hii ni baada ya Rais Yahya Jammeh amekataa koundoka madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi.

Rais wa Senegal Macky Sall, Ellen Johnson Sirleaf (Liberia), Makamu Rais wa Sierra Leone Victor Foh pamoja na aliyekuwa rais wa Ghana John Mahama watasafiri kwenda Abuja kwa Mazungumzo.

Bwana Buhari na Rais wa zamani wa ghana John Mahama pia wamepewa jukumu na Jumuia ya nchi za Afrika Magharibi, Ecowas, kuhakikisha usalama wa mshindi wa uchaguzi Adama Barrow, na pia kuhakikisha kuwepo upokezanaji wa amani wa mamlaka tarehe 9 mwezi Januari.

Bwana Buhari na viongozi wengine wa nchi za Afrika Magharibi walimtembelea bwana Jammeh mwezi uliopita lakini hawakufanikiwa kumshawishi kuondoka madarakani

Maafisa wa Ecowas wanasema kuwa hatua za kijeshi za kumlazimisha Jammeh kuondoka madarakani zinafanyiwa tathmini.

Mkuu wa majeshi nchini Gambia ametangaza kumuunga mkono bwana Jammeh na ripoti zingine zinasema kuwa amekuwa na mpango wa kuwaajiri mamluki kutoka nchini Liberia na Ivory Coast.