Rais wa zamani wa Chad kukata rufaa

Habre alihukumiwa kifungo cha maisha jela Haki miliki ya picha AFP/getty
Image caption Habre alihukumiwa kifungo cha maisha jela

Mawakili wa rais wa zamani wa Chad Hissene Habre, wanatarajiwa kukata rufaa ya kupinga hukumu ya kifungo cha maisha kwa makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliotokea wakati wa kipindi cha utawala wake miaka ya themanini.

Haijulikani ikiwa bwana Habre atahitajika kufika mahakamani yeye binafsi kwenye mji mkuu wa Senegal Dakar, makahama ambayo haiitambui.

Hukumu yake ya mwezi May ilionekana kama ushindi mkubwa dhidi ya ukwepaji sheri unaoshuhudiwa miongoni mwa viongozi dhalimu wa nchi za Afrika.

Inakadiriwa kuwa hadi watu 40,000 waliuawa nchini Chad wakati wa uongozi wa raia Hissein Habre huku maelfu wakibakwa na kuteswa.

Kusikilizwa kwa rufaa kunatarajiwa kuchukua siku kadha.