Ukosefu wa umeme waikumba Kenya

Mtambo wa umeme
Image caption Mtambo wa umeme

Maeneo kadha nchini Kenya yamekumbwa na ukosefu wa nguvu za umeme tangu Jumapili jioni kutokana na kile kinachotajwa kuwa tatizo la kiufundi.

Hali kama hiyo ilishuhudiwa mwaka uliopita ambapo kampuni ya pekee ya kutoa huduma za umme nchini Kenya, ilisema kuwa hitilafu hiyo ilisababishwa na nyani.

Maeneo yaliyoathiriwa na ukosefu huo wa nguvu za umeme ni pamoja na mji wa Nairobi , maeneo ya pwani na kaskazini mwa nchi.

Mji wa viwanda wa Thika yaliko makampuni makubwa iwemo kampuni ya kuunda magari ya Volkswagen pia nao umeathiriwa.

Nguvu hizo za umeme zilipotea wakati wa hafla iliyokuwa ikihudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta hiyo jana, hadi kusababisha kutafutwa kwa nishati mbadala baada ya mataa kuzima.