Ouattara afukuza wakuu wa majeshi, baada ya uasi

Wanajeshi wa Ivory Coast Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanajeshi wa Ivory Coast

Siku ya Ijumaa wanajeshi wenye chuki waliasi katika mji wa Bouake, kabla ya vikosi vya jeshi vilivyo katika kambi kwenye miji mingine kuunga mkono hatua hiyo.

Uasi huo wakitaka nyongeza ya mshahara, ulimalizika baada ya Rais Ouattara kukubali matakwa yao.

Taarifa kutoka Ikulu ya nchi hiyo inasema Mkuu wa Majeshi, mkuu wa jeshi la polisi wameachishwa kazi mara moja.