Maelfu wahudhuria mazishi ya Rafsanjani

Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei(wa pili kulia) na Rais Hassan Rouhani(kati kati) wakiguza jeneza la Akbar Hashemi Rafsanjani Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei(wa pili kulia) na Rais Hassan Rouhani(kati kati) wakiguza jeneza la Akbar Hashemi Rafsanjani

Maelfu ya watu nchini Iran wamejitokeza kwenye mji mkuu Tehran kwa mazishi ya rais wa zamani Akbar Hashemi Rafsanjani.

Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei aliongoza maombi kwenye sherehe hizo.

Rafsanjani ambaye alikuwa rais kati ya mwaka 1989 na 1997 aliaga dunia kutoka na mshutuko wa moyo siku ya Jumapili akiwa na umri wa maika 82.

Alikuwa mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa tangu yafanyike mapinduzi ya mwaka 1979.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Raia wakiwa na picha za Akbar Hashemi Rafsanjani mjini Tehran

Televisheni ilionyesha umati mkubwa wa waombolezaji katika mitaa inayozunguka chuo kikuu cha Tehran ambapo maombi yanafanyika.

Haki miliki ya picha Reuters
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rafsanjani alikuwa muungaji mkono wa rais wa sasa wa Iran Hassan Rouhani
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Raia wa Iran wakikusanyika kando ya gari lililokuwa limebeba jeneza la Rafsanjani mjini Tehran.