Mike Tyson kumfunza Chris Brown kumpiga Soulja Boy

Mike Tyson Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mike Tyson anasema atamfunza Chris Brown

Mike Tyson amethibitisha kuwa atampa mafunzo Chris Brown kwa pigano lake kufuatia mzozo na mwanamuziki Soulja Boy.

Mwanamasumbwi huyo bingwa wa uzani wa juu aliombwa na mwanamuziki 50 Cent, kufuatia mzozo mbaya kati ya Chris Brown na Soulja Boy wiki chache zilizopita.

Nitamfunza vile atauma sikio la mtu," alisema Mike Tyson.

"Nitamfunza kila mbinu chafu. Kwa sababu siwezi kumfunza jinsi ya kukimbia."

Soulja Boy anafunzwa na bingwa mwingine wa ndondi, Floyed Mayweather.

Pigano hilo la raundi tatu litafanyiwa huko Las Vegas tarehe ambayo haijatangazwa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Chris Brown

Mzozo huo ulianza pale Soulja Boy aliandika maoni chini ya picha ya Karrueche Tran, ambaye ni mpenzi wa zamani wa Chris Brown.

Wote hao walinza kuchapisha picha na video za kutishana.

Soulja Boy ndiye aliandika kuhusu pigano hilo lakini akaondoa ujumbe huo badaye.

50 Cent amemuanga mkono Soulja Boy na kusema kuwa atatoa dola laki moja kwa matokeo ya pigano hilo.

Chris Brown wa umri wa miaka 27 na Soulja Boy 26, wamekosolewa na wasanii wengine kwa kuzozana hadharani.

Soulja Boy aidha analaumiwa kwa kutumia pigano hilo kama njia ya kufufua taaluma yake ya muziki inayofifia.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Soulja Boy