Mzozo kuhusu kiwanda cha mkaa Lamu, Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Mzozo kuhusu kiwanda cha makaa ya mawe Lamu, Kenya

Ujenzi wa kituo cha kuzalisha nishati kupitia makaa ya mawe eneo la Lamu, pwani ya Kenya umezua zogo kubwa huku baadhi ya wakazi wa Lamu wakiupinga vikali.

Wanasema mradi huo utawadhuru kiafya na kuvuruga biashara yao ya samaki.

Kituo hicho kitajengwa eneo la Kwasasi, kilomita 21 kutoka mji wa Lamu, na kusimamiwa na kampuni ya Amu Power huku ujenzi ukitekelezwa na kampuni ya Investment and Power Contsurction Corporation kutoka China.

Mwandishi wa BBC John Nene anaarifu.

Mada zinazohusiana