Kesi ya uchaguzi wa Gambia yahairishwa hadi Mei

President Jammeh after voting in December Haki miliki ya picha AFP
Image caption Yahya Jammeh has governed The Gambia for 22 years

Mahakama ya juu zaidi nchini Gambia haiwezi kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya kura ya mwezi uliopita hadi mwezi Mei , kwa mujibu wa jaji mkuu Emmanuel Fagbenle.

Kiongozi wa muda mrefu Yahya Jammeh mwenye umri wa miaka 51 awali alikubali kushindwa lakini baadaye akakataa matokeo hayo.

Bado haijulikani kitakachotokea baada ya muhula wa bwana Jammeh kukamilika tarehe 18 mwezi Januari.

Rais mteule Adama Barrow anasubiri kuapishwa siku ambayo itafuatia. Lakini bwana Jammeh anasema kuwa hawezi kuondoka madarakani na ana uungwaji mkono wa mkuu wa majeshi.

Viongozoi wa nchi za Afrika wakiongozwa na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari wanatarajiwa kuwasili mji mkiu wa Gambia Banjul siku ya Jumatano katika jitihada za kutaua mzozo uliopo.

Jammeh amepinga jitihada zao akisema kuwa hawana haki ya kuingilia masuala ya nchi yake.

Kuhusu BBC