Emmanuel Bushayija atangazwa mfalme mpya wa rwanda

Mfalme Kigeli V Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mfalme Kigeli wa Rwanda aliongoza kwa muda mfupi kabla ya kulazimishwa kukimbilia uhamishoni

Mwanamume wa miaka 56, mkazi wa Uingereza na ambaye wakati mmoja alifanya kazi katika kampuni ya vinywaji nchini Uganda ametawazwa kuwa mfalme mpya wa Rwanda akiwa uhamishoni.

Mwanamfalme Emmanuel Bushayija amechukua nafasi ya babu yake Mfalme Kigeli V, ambaye alifariki nchini Marekani mwezi Oktoba mwaka jana akiwa na umri wa miaka 80.

Taarifa kutoka kasri ya mfalme zinaarifu kuwa mfalme mpya alilelewa akiwa uhamishoni Uganda na baadaye akafanyia kazi kampuni ya vinywaji ya Pepsi Cola katika mji mkuu wa Kampala.

"Baadaye alijiunga na sekta ya utalii nchini Kenya, kabla ya kurejea Rwanda kati ya mwaka 1994 na 2000. Tangu wakati huo mfalme mpya aliishi Uingereza ambapo alioa na kujaaliwa na watoto wawili," taarifa hiyo imesema.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii