Taiwan imesema inadadisi hatua hiyo ya China

Meli ya china Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Meli hiyo ilikuwa inatoka mazoezini kwa mara ya kwanza.

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema ndege ya kipekee ya Uchina imeongoza meli kadhaa za kivita kuingia eneo hilo.

Ndege hiyo ilikuwa inarejea kutoka mazoezini kusini mwa bahari ya China.

Hii ni mara ya kwanza kwa China kuchukuwa hatua hiyo licha ya mvutano unaoendelea kujitokeza baina ya majirani hao wawili. Utawala wa Taiwan hatahivyo umetoa wito kwa watu wake kuwa watulivu.

Mkuu wa baraza la masuala ya kisiwa hicho, Chang Hsiao-Yueh, amesema usimamizi wake unafuatilia kwa makini hatua ya China.

"Nasisitiza kwamba serikali ina uwezo wa kulinda usalama wetu wa kitaifa. Kwa hiyo hakuna haja ya kuwa na hofu."

China imeongeza shughuli zake za kijeshi karibu na Taiwan. Mara kadhaa taifa hilo limenukuliwa likuzungumzia uhusiano wake na kisiwa hicho kuwa wa kuyumba yumba.

Mzozo wa kidiplomasia ulizuka baada ya Bi Tsai kuzuru Marekani wikendi iliyopita akiwa njiani kuelekea Amerika ya Kati, na kukutana na maafisa wa taifa hilo licha ya Beijing kutoridhishwa na hatua hiyo.