Trump apinga madai mapya kuhusu Urusi

Donald Trump Haki miliki ya picha AP
Image caption Donald Trump

Urusi imetupilia mbalia ripoti kuwa inamiliki taarifa za siri kumhusu Donald Trump kuwa uongo na jaribio la kuharibu uhusiano kati ya Urusi na Marekani.

Ripoti zinazosambaa kwenye vyombo vya habari nchini Marekani zinasema kuwa Urusi ina taarifa chafu kuhusu biashara za Trump na kanda ya video kuhusu maisha yake binafsi.

Akijibu kupitia mtandao wa twitter Trump alitaja ripoti hizo kuwa zisizo za kweli.

Maafisa nchini Marekani wanasema kuwa idara za ujasusi zimejulisha bwana Trump na Rais Obama kuhusu madai hayo.

Bwana Trump anatarajiwa kufanya mkutano na waandishi wa habari leo Jumatano siku tisa kabla ya kuingia ofisini.

Mkutano huo unatarajiwa kuwa wa Trump kutangaza kujitenga kutoka bishara zake.

Vyombo vya habari vinaripoti kuwa Urusi pia ina taarifa kuhusu mawasiliano ya siri kati ya timu ya kampeni ya Trump na Urusi.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Vinyago vya Putin and Trump