Marekani imesema huenda isizuie makombora ya Korea Kaskazini

Mr Carter alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wake wa mwisho na waandishi habari Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mr Carter alikuwa akizungumza wakati wa mkutano wake wa mwisho na waandishi habari

Waziri wa ulinzi nchini Marekani Ash Caret amesema kuwa Marekani haiwezi kulizuia kombora la Korea Kaskazini ikiwa halitishii chochote.

Amasema kuwa jeshi la Marekani litahiitaji kupata taarifa zaidi kuhusu kombora hilo baadala ya kukabiliana nalo.

Matamshi hayo yanajiri baada ya rais mteule Donald Trump kuuzungumzia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini kwenye mtandao wa Twitter.

Trump alikuwa amesema kuwa mopango ya Korea Kaskazin ya kuunda kombora linaloweza kufika nchini Marekani haitafanyika.

Hata hivyo hakufafanua vile anaweza kukomesha mipango hiyo.

Wakati wa hotuba yake ya mwaka mpya, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, alisema kuwa nchi hiyo imefikia hatua za mwisho mwisho za kuunda kombora la masafa marefu.

Bwana Carter alisema wakati wa mkutano wake wa mwisho na waandishi wa habari kuw ikiwa kombora la masafa marefu la Korea Kaskazini litaonekana kuwa hatari litakabiliwa.

Bwana Carter anatarajiwa kuondoka ofisini kama mkuu wa ulinzi nchini Marekani wakati Rais Obama anakamilisha muhula wake mnano tarehe 20 mwezi huu.

Siku ya Jumapilia vymbo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini vilinukuu wizara wa mashauri ya nchi za kigeni ikisema kuwa kombora litarushwa wakati wowote na mahali popote kulingana uamuzi wa nchi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kim Jong-un amesema kuwa nchi hiyo imefikia hatua za mwisho mwisho za kuunda kombora la masafa marefu.