Upinzani waungana nchini Kenya

Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi kushoto, Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga na Katibu mkuu wa chama cha KANU Nick Salat wameazimia kuungana kwa vyama vyote vya upinzani nchini Kenya
Image caption Kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi kushoto, Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga na Katibu mkuu wa chama cha KANU Nick Salat wameazimia kuungana kwa vyama vyote vya upinzani nchini Kenya

Baada ya uvumi kuenea kuwa upinzani ulikuwa na mikakati ya kuunda muungano mmoja, sasa viongozi hao wamethibitisha kauli hiyo leo katika ukumbi wa Bomas mjini Nairobi.

Kwa mara ya kwanza, viongozi hao wameandaa hafla ya pamoja kuonyesha umoja wao na kutangaza mipangi hiyo rasmi.

Aliyekuwa Waziri mkuu, na kinara wa mrengo wa upinzani, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Kiongozi wa Chama cha ANC maarufu Amani, Musalia Mudavadi, wameungana I ili kutamfuta mgombea mmoja atayewakilisha upinzani ili kukabiliana na rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.

Zaidi ya vyama kumi vimethibitisha kuungana na kutangaza kuwa hiyo ndio njia pekee ya kuiondoa serikali iliyo mamlakani ikiongozwa na rais Uhuru Kenyatta.

Aidha, viongozi hao wameahidi lengo lao ni kuboresha hali ya taifa hilo wakidai kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu chini ya utawala wa sasa.

Image caption Wanachama wa chama cha upinzani cha Wiper nje ya ukumbi wa Bomas mjini Nairobi

Hata hivyo, hawakutangaza ni nani atayekuwa mgombea wao wa Urais, Uamuzi ambao unatarajiwa baada ya wiki kadhaa.

Vinara wa vyama hivyo, wametoa wito wa kumuunga mkono atakayeteuliwa kuwania urais kupitia mrengo huo kwani ndio hatua pekee ya kuimarisha umoja wao.

Viongozi hao wametumia mifano ya mataifa ya Afrika kama Ghana na Gambia ambapo umoja wa upinzani umeweza kuwaletea ushindi.

Kuhushu sheria ya uchaguzi iliyokarabitiwa, viongozi hao wameahidi kufanya mgomo baada ya shughuli ya kuwaandikisha wapiga kura inayatorajiwa kuanza nchini humo wiki ijayo, kumalizika.

Wamewahimiza wafuasi wao kujiandikisha kwa idadi kubwa ili kuzidisha nafasi zao za kupata ushindi.