Mkimbizi kutoka Somalia ateuliwa waziri Canada

Ahmed Hussen (kati kati) Haki miliki ya picha AP
Image caption Ahmed Hussen (kati kati)

Waziri mkuu nchini Canada Justin Trudeau amemteua Ahmed Hussen ambaye ni mkimizi wa zamani kutoka nchini Somalia kuwa waziri wa uhamiaji, wakimbizi na uraia.

Mwaka mmoja uliopita Bwana Hussen alikuwa akisherehekea, baada ya kuwa msomali wa kwanza kuwa mbunge nchini Canada.

Sasa amepanda cheo na kuwa mtu wa kwanza mwenye asili ya Somalia kuwa waziri.

Aliingia nchini Canada kama mkimbizi kutoka mjini Mogadishu miongo miwili iliyopita akiwa na umri wa miaka 16.

Canada tayari ina sheria nzuri kwa wakimbizi na ilkiwapa makao karibu raia 40,000 wa Syria mwaka uliopita.