Viongozi wa ECOWAS wamfuata Jammeh, kusuluhisha

Rais Jammeh na viongozi wa Ecowas Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais Jammeh na viongozi wa Ecowas

Viongozi wa Jumuia ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS wanatarajiwa kuwasili Gambia, kukutana na rais wa nchi hiyo Yahya Jammeh kesho Ijumaa.

Ziaka ya viongozi hao inafuatia hatua ya rais Jammeh ya kung'oma kuondoka madarakani hata baada ya kushindwa katika uchaguzi.

Kabla ya kukutana na viongozi hao Rais Jammeh ametoa hotuba kwa taifa, akizungumzia uamuzi wa Mahakama kuu kuahirishashauri lake kuhusiana na uchaguzi wa nchi hiyo.

Katika hotuba hiyo amezionya jumuia za kimataifa, ikiwemo Umoja wa Afrika na ECOWAS, kutoingilia masuala ya nchi yake.

Hata hivyo, inaripotiwa kwamba hali imeanza kuwa tete nchi humo huku baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu wameanza kugoma kama njia moja wapo ya kumshinikiza rais Jammeh kuachia madaraka.

Huyu hapa ni mmoja wa wanafunzi hao:

"wazazi wetu wanataka tumalize masomo yetu, baadhi yetu tuko mwaka wa mwisho wa masomo. Kwa hiyo wana wasi wasi na usalama wetu, na hawafurahii kutuona tumesusia masomo, ingawa wanaamini kwamba tunajukumu la kufanya hivyo."

Nae mkufunzi wa chuo kikuu cha Gambia alikuwa na haya ya kusema:

"Ukiangalia vizuri, utaona kwamba Chuo Kikuu Cha Gambia kwa mara nyengine, kimejua kwamba jukumu lake sio kuwa na wasomi pekee, bali kuwa na wasomi ambao wanawajibika kwa jamii nzima ya Gambia.