Urusi kupiga marufuku uvutaji sigara kwa watu wanaozaliwa baada ya 2014

Urusi kupiga marufuku uvutaji sigara Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Urusi kupiga marufuku uvutaji sigara

Wiazara ya afya nchini Urusi inatathmini kuweka mafuruku ya kuzua uuzaji wa sigara kwa watu waliozaliwa mwaka 2014 au baadaye.

Ni moja ya mikakati mikali ya kukabiliana na matumizi ya bidhaa za tumbaku ambayo wanasiasa wa nchi hiyo wanataka kutekeleza.

Marufuku ya kuuza bidhaa za tumbaku kwa kizazi hiki na kile kinachokuja itaendelea hadi wakati watakuwa watu wazima.

Sheria hiyo inafanyiwa tathmini kwa wakati huu lakini ina maana kuwa uvutajia sigara utakuwa haramu kwa raia wote wa Urusi.

Makundi yanayopinga matumizi ya tumbaku yametaka hatua kama hizo kuchukuliwa sehemu zingine za dunia lakini hawajawapata uungwaji mkono wa serikali.

Uvutaji sigara tayari ni haramu katika maeneo ya kazi nchini Urusi, makazi ya watu, kwenye mabasi, treni na umbalia wa mita 15 kutoka vituo vya treni na viwanja vya ndege.

Urusi ina moja ya viwango vya juu vya uvutaji sigara duniani wakati karibu asilimia 40 ya raia wake wakiwa wanavuta sigara.

Katika baadhi ya maduka pakiti ya sigara ianweza kuuzwa kwa chini ya dola moja.

Soko la sigara nchini Urusi linakadiriwa kuwa la thamani ya dola bilioni 22.

President Putin havuti sigara na mara nyingi amewashutumu mawazir kwa kuvuta sigara

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Putin havuti sigara na mara nyingi amewashutumu mawazir kwa kuvuta sigara