Nyota wa filamu Idris Elba ajinadi siku ya Valentine

Msanii wa filamu Idris Elba amejinadi siku ya wapendanao ya Valentine ili kuchangisha fedha za hisani. Haki miliki ya picha OMAZE.COM
Image caption Msanii wa filamu Idris Elba amejinadi siku ya wapendanao ya Valentine ili kuchangisha fedha za hisani

Msanii wa filamu Idris Elba amejinadi siku ya wapendanao ya Valentine ili kuchangisha fedha za hisani.

Katika kanda ya video iliochezwa mitandaoni ,amesema kwamba watakaochangisha fedha atawaburudisha kimepenzi katika usiku wa siku ya Valentine ikiwemo vinywaji, chakula na ''kile mtu atakachopenda''.

Amesema fedha za mchango huo zitaelekezwa kwa mashirika ya hisani yanayofanya kazi kuwasaidia wasichana barani Afrika.

Mshindi atajiunga na Elba katika chakula cha jioni cha 'Candlelit' katika mkahawa mmoja aupendao .

Usafiri wa ndege, malazi na hoteli yenye hadhi ya nyota nne vitakuwemo kulingana na nyota huyo katika mtandao wake wa Omaze.

Wanaotaka kushiriki wana hadi tarehe 14 mwezi Februari kuwasilisha maombi yao.

Elba aliweka sauti katika filamu ya Shere Khan kwa jina Jungle Book mbali na kutayarisha na kuigiza katika filamu ya Beats of No Nation 2015.

Pia anatarajiwa kuigiza katika filamu ya The Dark Tower mwaka huu, filamu ya kutisha itakayoshirikisha msururu wa vipindi vya kitabu cha Stephen King.