Vipimo vya onyesha Kuenea kwa saratani kumepungua kwa 75%

Mapafu ya binadamu Haki miliki ya picha SPL
Image caption Jopo la wanasayansi katika taasisi ya Sanger ya Cambridge walikuwa wakijaribu kubaini nini kiini cha kusambaa kwa uvimbe mwilini.

Kuenea kwa maradhi yanayouwa ya saratani katika maeneo ya mwili kumepunguzwa kwa robo tatu katika vipimo walivyofanyiwa wanyama , wanasema wanasayansi.

Uvimbe wa saratani unaweza "kuota" wenyewe katika sehemu yoyote ile ya mwili na mchakato huu ndio unaosababisha asilimia 90% vifo vitokanavyo na saratani.

Utafiti uliofanywa kwa panya, uliochapishwa na jarida la Nature, ulionyesha kuwa kuvuruga mfumo wa kinga kulipunguza kasi ya kuenea kwa saratani za ngozi na mapafu.

Kituo cha utafiti wa saratani cha Uingereza kimesema kuwa matokeo ya uchunguzi wa awali yametoa taswira mpya kuhusu namna uvimbe wa saratani unavyosambaa na inaweza kuwezesha upatikanaji wa tiba mpya.

Kuenea kwa saratani - kunakofahamika kama metastasis - kwa lugha ya kitaalam ni vita baina ya kuenea haraka kwa saratani na maeneo mengine ya mwili.

Haki miliki ya picha SPL
Image caption Panya walichomwa sindano yenye saratani ya mwili (melanomas) na kisha jopo la wanasayansi lilihesabu idadi ya uvimbe uliojitokeza kwenye mapafu yao

Jopo la wanasayansi katika taasisi ya Sanger ya Cambridge walikuwa wakijaribu kubaini nini kiini cha kusambaa kwa uvimbe mwilini.

Watafiti walibuni vitengo 810 vya vinasaba vya panya wa jamii moja ili kuvumbua ni kitengo gani cha vinasaba(DNA) kilikuwa na mwili ulioweza kuzuwia kusambaa kwa saratani.

Wanyama walichomwa sindano yenye saratani ya mwili (melanomas) na kisha jopo la wanasayansi lilihesabu idadi ya uvimbe uliojitokeza kwenye mapafu.

Uchunguzi wao uliwawezesha kugundua kuwa vitengo 23 vya vinasaba (DNA), ama gini, ambazo ziliwezesha kuwa rahisi ama vigumu kwa saratani kuenea mwilini.

Nyingi kati ya gini zilihusika katika kudhibiti mfumo wa kinga ya mwili.

Kulenga moja ya gini - inayoitwa Spns2 -kulipelekea kupungua kwa theluthi tatu ya kusambaa kwa uvimbe kwenye mwingi kwenye mapafu.

Dokta Justine Alford, kutoka Taasisi ya utafiti wa saratani nchini Uingereza, amesema: "uchunguzi huu katika panya wa maabara unatoa taswira mpya katika gini ambazo zinahusika kwa kiasi kikubwa katika kuenea kwa saratani mwilini na unaweza kuwa njia ya kutibu saratani siku zijazo.

"saratani ambayo imesambaa ni ngumu kutibu, kwa hiyoutafiti kama huu ni muhimu katika kutafuta njia za kushughulia mchakato huu ."amesema Dokta Alford.