Stevie Wonder amemuimbia Michelle Obama katika kipindi cha TV

Stevie Wonder Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Stevie Wonderalianza kwa kusema : "Nakupenda , Michelle."

Stevie Wonder amemuimbia mke wa rais wa Marekani Michelle Obama, ambapo alibadilisha maneno ya nyimbo zake mbili kama heshima kwake wakati anapojiandaa kuondoka katika ikulu ya White House.

Bi Obama alishiriki katika kipindi cha usiku cha Televisheni kama mke wa rais cha Jimmy Fallon kwenye televisheni ya NBC Jumatano.

Alisema Wonder ndie muimbaji anayempenda, na aliletwa ili kumuimbia bi Michelle katika kipindi hicho maarufu cha Fallon's Tonight Show.

Aliimba nyimbo zake - Isn't She Lovely and My Cherie Amour, akibadilisha kwa maneno "My Michelle Amour".

Haki miliki ya picha AP
Image caption Michelle Obama amekuwa mgeni wa mara kwa mara katika kipindi cha televisheni cha Jimmy Fallon

Pia alibadilisha maneno katika nyimbo zake nyingine , kama vile "How I wish that you were mine" na kuwa "You'll always be first lady in our life".

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mke wa rais pia aliimba baadhi ya nyimbo hizo pamoja na Jerry Seinfeld, Fallon na Dave Chapelle

Mke wa rais Obamaamekuwa katika ikulu ya White House na mumewe Barack kwa miaka minane .Rais anayeingia madarakani Donald Trumpataapishwa tarehe 20 Januari.

Wonder alianza alipotokea kwenye kipindi cha The Tonight alisema "nakupenda , Michelle,"kabla ya kuanza kumuimbia wimbo - Isn't She Lovely, ambapo alibadilisha kibwagizo katika wakati mmoja na kuimba : "Michelle is lovely."

Wakati wa kipindi hicho, Bi Obama pia alikuwa akiimba nyimbo hizo pamoja na msanii wa vichekesho Dave Chapelle na Jerry Seinfeld, jambo lililoshangaza hadhila iliyokuwa imrekodia ujumbe wake wa kuaga.

Bi Obama amekuwa mgeni wa mara kwa mara wa wa kipindi cha The Tonight Show na mualikwa wa kipindi cha awali cha Late Night pamoja na Jimmy Fallon.

Mada zinazohusiana