Mteja atoa bakshishi ya £1000 kwa chakula cha £79

Wafanyikazi wa mkahawa huo watagawanyiwa bakshishi hiyo kulingana na mmiliki wa mkahwa huo Luna Ekush, kushoto Haki miliki ya picha PORTADOWN TIMES
Image caption Wafanyikazi wa mkahawa huo watagawanyiwa bakshishi hiyo kulingana na mmiliki wa mkahwa huo Luna Ekush, kushoto

Mteja mmoja aliyekula chakula cha jioni katika mkahawa mmoja nchini India katika huko Portadown amewashangaza wafanyikazi wa mkahawa huo kwa kuwacha bakshishi ya pauni 1000 kwa malipo ya chakula cha pauni 79.

Chef babu, Shabbir Satter wa mkahawa wa India Tree mjini humo alisema kuwa mtu huyo ambaye jina lake alitaka libanwe alimuita '' busara''.

Mteja huyo ni miongoni mwa kundi la wageni watano waliokula katika mkahawa huo Jumanne iliopita, gazeti la Portadown liliripoti.

Amesema kuwa angependa kupongeza chakula kizuri alichopata.

Luna Ekush ,ambaye anamiliki mkahawa huo , alisema kuwa bakshishi hiyo ni ya ''ukarimu mkubwa''.

''Ni kitu kidogo sana kwa sisi kuonyesha shukran zetu, lakini hilo limekuwa na athari kubwa''.

''Bado tumeshangaa'',alisema.

Wafanyikazi wote waliokuwa wakifanya kazi usiku huo watagawanya fedha hizo kwa kuwa mteja huyo alisema ni za kila mtu.

''Sidhani kama kuna mtu aliyepokea kitita kikubwa kama hicho,mimi mwenyewe sijapata''.

''Nataka kumshukuru Babu kwa chakula chake kizuri, sifa zote zinamwendea yeye''.