Donald Trump: Nitashirikiana na Urusi na China

Rais mteule Donald Trump amesema kuwa yuko tayari kushirikiana na China na Urusi iwapo zitashirikiana naye
Image caption Rais mteule Donald Trump amesema kuwa yuko tayari kushirikiana na China na Urusi iwapo zitashirikiana naye

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kushirikiana na Urusi na China, iwapo mataifa hayo yatashirikiana naye.

Katika mahojiano na Wall street journal, bw Trump amesema vikwazo vilivyowekewa Urusi hivi majuzi, vitaendelea kuwepo, japo huenda vikaondolewa iwapo Urusi itasaidia Marekani katika vita dhidi ya ugaidi.

Anatumai kwamba atakuwa na kikao na rais Putin hivi karibuni.

Trump apinga madai mapya kuhusu Urusi

Urusi 'kuichokoza' Nato kabla Trump awe rais

Trump ampongeza Putin kwa kutolipiza kisasi

Trump: Putin anamshinda Obama kwa uongozi

Marekani yaapa kuichukulia hatua Urusi

Pia amesema kuwa sera ya One China ambayo Marekani haitambui Taiwan itajadiliwa upya.

Wakati huohuo kamati ya bunge la seneti nchini Marekani imetangaza kwamba itachunguza madai kwamba urusi iliingilia uchaguzi wa Marekani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii