Michuano ya kombe la Afrika kung'oa nanga Gabon

Michuano ya kombe la bara Afrika kung'oa nanga nchini Gabon
Image caption Michuano ya kombe la bara Afrika kung'oa nanga nchini Gabon

Michuano ya kombe la mataifa ya bara Afrika 2017 inaanza Jumamosi nchini Gabon huku waandalizi hao wakikabiliana na Guinea-Bissau.

Katika kipindi cha siku 23 timu 16 zitachuana kuwania kombe hilo lenye umaarufu mkubwa barani.

Mechi hizo zilitarajiwa kufanyika nchini Libya ,lakini vita vya wenyewe kwa wenyewe viliwalazimu wasimamizi kubadili nia na kuelekea Gabon ambayo iliandaa michuano hiyo mwaka 2012.

Waandalizi hao ndio timu ya pekee ambayo imeorodheshwa katika nafasi ya chini, lakini katika mchuano ambao 'mpira hudunda' huenda wakafika nusu fainali.

Misri, Algeria, Senegal na Ghana ni miongoni mwa timu zainazopigiwa upatu kushinda kombe hilo.