Kufutwa kwa Mourinho kuliigharimu Chelsea £8.3m

Jose Mourinho Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jose Mourinho

Kupigwa kalamu kwa aliyekuwa mkufunzi wa Cheslea Jose Mourinho na maafisa wake mwaka 2015 kuliigharimu Chelsea pauni milioni 8.3 kama fidia kulingana na takwimu zilkizotolewa na klabu hiyo.

Mourinho ,ambaye sasa anaifunza manchester United alifutwa mwezi Disemba baada ya matokeo mabaya ya mabingwa hao watetezi msimu huo.

Klabu hiyo ilimaliza katika nafasi ya 10 huku ripoti ya mayumizi ya fedha ikionyesha hasara ya pauni milioni 70.6.

Hiyo inashirikisha gharama ya pauni milioni 67 iliotumika kuilipa kampuni ya Adidas ili kufutilia mbali kandarasi ya ufadhili.

Klabu hiyo iifanya hivyo na kuingia katika kandarasi na kampuni ya Nike ambayo ilikuwa na thamnai ya ya zaidi ya dola milioni 30 kwa mwaka.

Kandarasi hiyo ya Adidas ambayo Chelsea iliikatiza miaka sita iliopita ilikuwa ya thamani ya pauni milioni 30 kwa mwaka.