John Kerry azuru eneo ambapo alimuua hasimu Vietnam

John Kerry akiwa eneo ambapo alipigana vita vya Vietnam Haki miliki ya picha AFP / Getty Images
Image caption John Kerry akiwa eneo ambapo alipigana vita vya Vietnam

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Marekani anayeondoka John Kerry, amezuru eneo moja nchini Vietnam, ambapo alivamiwa wakati wa Vita vya Vietnam.

Kerry mwanajeshi mwanamaji wa zamani alikutana na mpiganaji wa zamani wa Vietnam mwenye umri wa miaka 70 ambaye anakumbuka shambulizi hilo la mwaka 1969.

Wawili hao walisalimiana kwa mikono

Bwana Kerry ambaye yuko nchini Vietnam kwa ziara yake ya mwisho kabla ya kuondoka ofisini, alitunukiwa kwa ujasiri wake vitani.

Kerry alimuambia hasimu wake huyo wa zamani Vo Ban Tam, kuwa ni vizuri wote wako hai.

Bwana Tam ambaye sasa ni mkulima, anasena anafahamu mtu ambaye Kerry alimuua na pia anakumbuka njama yao ya kushambulia mashua ya Marekani.

Kerry ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 26, alitunukiwa kwa kukinusuru kikosi chake baada ya kumpiga risasi na kumuua mtu ambaye alikuwa akipanga kushambulia mashua yao kwa kombora.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption John Kerry (kushoto) akizungumzanna mpiganaji wa Vietnam Vo Ban Tam (wa pili kulia)
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption John Kerry akitumia ramani kutambua eneo ambapo shambulizi lilitokea
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption John Kerry akindamana na mwanahistoria Edward Miller